Waziri Mkuu wa China ahimiza makampuni ya China na UAE kutumia vizuri fursa mpya za ushirikiano
2024-09-13 14:12:46| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang aliyeko ziarani katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Alhamisi alitoa wito kwa makampuni ya China na UAE kutumia vizuri fursa mpya za ushirikiano chini ya jitihada imara za pamoja za nchi mbili.

Li alisema hayo alipohutubia Kongamano la Viwanda na Biashara la UAE na China. Alisema uhusiano kati ya China na UAE uko katika kipindi muhimu cha kihistoria, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi mbili unakaribisha fursa muhimu ya kuboreshwa. Anataka makampuni ya nchi mbili yafuate mwelekeo mkuu na kushikilia fursa mpya za ushirikiano.