China na Zambia zasaini makubaliano ya utaratibu wa hospitali mwenza
2024-09-13 09:28:20| CRI

China na Zambia jana Alhamisi zimetangaza utaratibu wa ushirikiano wa hospitali mwenza kati ya Kamsheni ya Taifa ya Afya ya China na Wizara ya Afya ya Zambia.

Makubaliano hayo yatawezesha hospitali tanzu ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Zhengzhou cha China na hospitali ya mafunzo ya Chuo Kikuu cha Levy Mwanawasa cha Zambia kuanzisha utaratibu wa ushirikiano katika nyanja ya utaalamu wa matatizo ya tezi dume.

Balozi wa China nchini Zambia Han Jing amesema makubaliano hayo yatawezesha China kuisaidia Zambia kuimarisha ujenzi wa uwezo wa kufanya pasuaji za mfumo wa mkojo, kuingiza teknolojia za pasuaji zenye jeraha dogo (MIS), na kutuma kikundi cha wataalamu kutoa mafunzo na mwongozo kwa wafanyakazi wa afya katika vitengo vya pausaji za mfumo wa mkojo.