Makampuni mengi ya kigeni yaonesha imani na soko la China wakati maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya 2024 (CIFTIS) yakifungwa
2024-09-16 09:19:04| CRI

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya 2024 (CIFTIS) yamefungwa mjini Beijing, na kufikiwa kwa makubaliano 1,000 ya mikataba na uwekezaji, huku zaidi ya asilimia 20 ya waonyeshaji wake kwenye tovuti wakiwani kampuni za kimataifa.

Kampuni nyingi zinazofadhiliwa na nchi za kigeni zimeonesha ubunifu wao wa hivi karibuni, huku zikionyesha imani katika kuchunguza soko la China.

Matokeo yaliyopatikana kwenye maonyesho hayo kwa mwaka huu, ni pamoja na miamala na uwekezaji katika sekta mbalimvali kama vile ujenzi, fedha na huduma za biashara. Wakati wa maonesho hayo pia mikutano 56 ilifanyika, ikijumuisha mazungumzo ya mradi wa ushirikiano wa kimataifa na mikutano ya kukuza, kulingana na mratibu.

Jumla ya kampuni na taasisi 111, zikiwemo kampuni za Fortune Global 500 na viongozi wa sekta mbalimbali, walitangaza mafanikio 219 katika nsekta za akili bandia, afya na nyinginezo, likiwa ni ongezeko la 80 ikilinganishwa na maonesho yaliyopita.

Waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bo, amesema matokeo hayo yameonyesha nia thabiti ya China ya kuinua maendeleo ya hali ya juu kupitia ufunguaji mlango wa hali ya juu, na matokeo haya yanaonyesha uelewa mpana na muhimu kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kibiashara wa sekta ya huduma.