Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) zilifanya mkutano mkubwa katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya umma wa China asubuhi ya Septemba 14 ili kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Bunge.
Rais Xi Jinping, alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu, akisisitiza haja ya kuimarisha imani zaidi katika njia, nadharia, mfumo na utamaduni, kuendeleza demokrasia ya watu katika mchakato mzima na kuendelea kudumisha, kuboresha na kuendesha mfumo wa Bunge la Umma kufikia matokeo mazuri ili kupata uhakikisho thabiti wa kitaasisi kwa Chama na watu kufikia malengo yao katika safari mpya ya zama mpya.
Aidha rais Xi amesema kuwa katika miaka 70 iliyopita, mfumo wa bunge la umma chini ya uongozi wa Chama cha CPC umehakikisha kuwa nchi inaendelea kusonga mbele katika njia ya ujamaa. Umedhihirisha faida kubwa za kisiasa katika kuhakikisha Chama kinawaongoza wananchi kutawala nchi kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha wananchi wanakuwa watawala wa nchi, kudumisha maisha ya kisiasa ya uchangamfu na utulivu, kuhimiza utawala wa sheria katika nyanja zote za masuala ya utawala wa taifa na kulinda utulivu na amani ya muda mrefu.