Watu 41 wafamaji na wengine 12 waokolewa baada ya boti kuzama Kaskazini mwa Nigeria
2024-09-16 09:19:42| CRI

Miili karibu 41 imepatikana, na watu wengine 12 waliokolewa baada ya boti kuzama katika jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara, nchini Nigeria.

Mbunge wa kitaifa anayewakilisha eneo bunge la Gummi-Bukkuyum la Nigeria Suleiman Gummi amesema kuwa boti iliyobeba abiria na wafanyakazi zaidi ya 50 ilizama kwenye mto karibu na Gummi, mji wa eneo la serikali ya mtaa wa Gummi huko Zamfara, muda mfupi baada ya kuondoka ufukweni. Abiria hao walikuwa wakulima ambao walisafiri kila siku kwa boti hadi mashambani mwao katika jamii jirani. Mamlaka za eneo hilo zilisambaza haraka wafanyakazi kwenye eneo la tukio hilo, wakiwemo wapiga mbizi, ambao waliwaokoa manusura zaidi ya kumi.

Mkuu wa Shirika la Usimamizi wa Majanga wa Jimbo la Zamfara Hassan Daura amesema kuwa wengi wao wakiwemo wanawake na watoto walikufamaji katika tukio hilo.

Ajali za boti zinaripotiwa mara kwa mara nchini humo na mara nyingi zinasababishwa na kujaza mizigo kupita kiasi, hali mbaya ya hewa na hitilafu za uendeshaji.