Kenya yasema uchumi wake wa mwaka huu utakua kwa asilimia 5.2
2024-09-17 08:58:35| CRI

Hazina ya Kitaifa ya Kenya imekadiria kuwa uchumi wake utakua kwa asilimia 5.2 mwaka 2024 na asilimia 5.4 mwaka 2025.

Katika Mapitio yake ya Bajeti na Waraka wa Mtazamo, Hazina imesema kuongezeka kwa uzalishaji wa kilimo na sekta ya huduma thabiti itasaidia ukuaji huo. Hali nzuri ya hewa na mipango ya serikali ya kuongeza nguvu za uzalishaji zitachochea kufufua sekta ya kilimo nchini Kenya. Aidha imesema sekta ya viwanda itashuhudia ukuaji mkubwa hasa kwa kupunguzwa gharama za uzalishaji na kupunguza shinikizo la viwango vya ubadilishaji wa fedha.

Hazina imeongeza kuwa sekta ya huduma itaendelea kuwa thabiti, na mageuzi katika sekta ya TEHAMA yatakuza ukuaji wa huduma za kifedha, afya na usimamizi wa umma.