Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imesisitiza mahitaji ya haraka ya Rwanda kushughulikia changamoto za kukuza ujuzi ili kudumisha ukuaji wake wa uchumi.
Katika ripoti yake mpya ya Uchumi wa Rwanda toleo la 23, yenye kichwa cha ‘Kuharakisha Ukuzaji wa Ujuzi Ili Kuchochea Ukuaji wa Sekta Binafsi’, inasisitiza umuhimu wa kuwapatia wafanyakazi ujuzi muhimu ili kukidhi mahitaji ya soko na kuchochea zaidi maendeleo.
Kwa mujibu ripoti hiyo, pato la taifa la Rwanda linatarajiwa kuwa na ukuaji wa wastani wa asilimia 7.6 kati ya mwaka 2024 na mwaka 2026. Hata hivyo, nguvu hii ya kiuchumi inaweza kudhoofishwa na ukosefu mkubwa wa ujuzi katika soko la ajira, wakati zaidi ya asilimia 62 ya makampuni yameripoti kuwa hayana programu ya mafunzo rasmi kwa wafanyakazi.