Muungano wa Chanjo Duniani (GAVI) umepanga kununua dozi 500,000 za chanjo ya Mpox kutoka kampuni ya Bavarian Nordic kwa ajili ya kusaidia kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika.
GAVI imepanga kutumia kiasi cha dola milioni 50 katika mpango huo, unaojumuisha usafirishaji, usambazaji na gharama za usimamizi wa chanjo.
Takribani dozi milioni 3.6 za chanjo ya Mpox tayari zimeahidiwa kutolewa na mataifa tajiri duniani kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini hadi sasa ni kiasi kidogo tu ambacho kimewasili.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mpaka sasa nchini DRC Congo kuna wagonjwa 25,000 wa Mpox huku jumla ya vifo 723 vinavyotokana na ugonjwa huo vikirekodiwa barani Afrika.