Waangalizi wa amani wa Sudan Kusini waridhia kuongezwa kipindi cha mpito kwa miaka miwili
2024-09-19 08:54:50| CRI

Tume ya Pamoja ya Ufuatiliaji na Tathmini (RJMEC) Jumatano iliuridhia utawala wa Sudan Kusini kuongeza kipindi cha mpito na kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu kwa miaka miwili ili kutekeleza makubaliano ya amani yaliyofufuliwa.

Mwenyekiti wa muda wa tume hiyo Charles Tai Gituai, alisema uamuzi wa serikali wa kuongeza kipindi cha mpito uliungwa mkono kwa kura 34 kati ya 41. Kwa mujibu wa ratiba mpya, nchi hiyo changa zaidi duniani itachagua viongozi katika uchaguzi mkuu wa kwanza kabisa Desemba 22, 2026, mwishoni mwa kipindi cha mpito.

Gituai alisisitiza kuwa wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi, kukabiliana na hali mbaya ya kiuchumi, ambayo inaendelea kuathiri maisha ya watu wa Sudan Kusini, ni kipaumbele cha kwanza, wakati mafunzo, umoja na kusambaza vikosi muhimu vya umoja pia ni muhimu.