Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza wasiwasi wake kutokana na ripoti za kuongezeka kwa mapigano katika mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini, El Fasher na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam iliyo karibu na mji huo.
OCHA imesema raia wengi wanaendelea kuathiriwa na mapigano hayo, pamoja na uhaba wa chakula uliothibitishwa katika eneo la Zamzam na maeneo mengine yaliyo hatarini zaidi, ambako si rahisi kufikiwa na misaada ya kibinadamu.
Ofisi hiyo imesema, Umoja wa Mataifa na wenzi wake wa kibinadamu wanaendelea kufanya juhudi kuwafikia watu walioko El Fasher, Greater Darfur na maeneo mengine nchini humo kuwapelekea msaada muhimu wa kuokoa maisha.