Ni wakati mwingine tena tunapokutana katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kila jumapili kupitia CGTN Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.
Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti itakayozungumzia Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia asema ushirikiano wa karibu zaidi na China unaleta manufaa kwa pande zote, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka CGTN Idhaa ya Kiswahili Nairobi ambayo yatahusu Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Viwanda yaliyoanza rasmi katika kituo cha maonyesho cha Sarit, Nairobi, nchini Kenya.