Hazina ya Marekani yapunguza viwango vya riba kwa alama 50, ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka minne
2024-09-19 08:55:29| CRI

Hazina ya Serikali ya Marekani Jumatano ilipunguza viwango vya riba kwa alama 50 kufuatia kupungua kwa mfumuko wa bei na kudhoofika kwa soko la ajira, ikiashiria kupunguzwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne.

Kamati ya Serikali ya Soko Wazi (FOMC) ilisema katika taarifa yake kwamba, kamati hiyo imepata imani kubwa zaidi kutokana na mfumuko wa bei kuendelea kushuka kuelekea asilimia 2, na hatari za kufikia malengo yake ya ajira na mfumuko wa bei zikiwa karibu katika uwiano. Hivyo kwa kuzingatia maendeleo hayo, kamati iliamua kupunguza lengo lake la kiwango cha fedha za serikali kwa alama 50 kuwa asilimia 4.75 hadi asilimia 5.

Baada ya kudumisha viwango vya juu kwa zaidi ya mwaka mmoja, sera ngumu ya fedha ya serikali ilikabiliwa na shinikizo la kubadilika kutokana na kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, ikiashiria kudhoofika kwa soko la ajira, na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi.