Wanawake na mchango wao katika sekta ya usanifu wa ujenzi
2024-09-20 08:38:34| CRI

Majukumu ya wanawake katika nyanja za usanifu na kubuni yamepuuzwa kwa muda mrefu kutokana na ubaguzi wa kijinsia. Kwa bahati nzuri, kuna mashirika ya kitaaluma ambayo yanasaidia wanawake katika kushinda vikwazo hivi vya jadi. Katika miaka ya hivi karibuni wamejitokeza wanawake wengi walioweza kuvunja dari ya kioo katika uwanja wa usanifu majengo, kuanzisha taaluma zenye mafanikio na kusanifu baadhi ya majengo ya kihistoria na mazingira ya mijini yanayovutia zaidi duniani.

Wanawake ni watu muhimu sana katika Usanifu na Kubuni. Jukumu wanalobeba katika usanifu wa majengo limekuwa likipuuzwa kihistoria. Mashirika mengi yamewasaidia wanawake kuondokana na vikwazo, kuanzisha kazi za usanifu wenye mafanikio, na kujenga majengo ya kihistoria na mazingira ya miji. Leo kwenye kipindi cha ukumbi wa wanawake tutaangalia mchango wa wanawake hawa katika sekta ya usanifu wa ujenzi pia tutawaletea simulizi ya msanifu mashuhuri wa China Lin Huiyin na pia Msanifu na mbunifu wa Ghana Lesley Lokko aliyeshinda tuzo ya medali ya dhahabu ya RIBA .