Maofisa na wataalamu wa nchini Ethiopia wameipongeza China kwa kuunga mkono ujenzi wa uwezo kwa Waethiopia, hususan vijana wa nchini humo.
Maofisa na wataalam hao wametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo uliozinduliwa jumanne wiki hii unaoitwa Seagull Talent Nurturing, ambao unalenga kuwawezesha vijana nchini Ethiopia kupitia mfumo wa utaratibu wa kuendeleza vipaji.
Maofisa hao pamoja na wataalamu wamesema China imekuwa ikichukua nafasi muhimu katika kuunga mkono maendeleo ya mafunzo ya ufundistadi na ujuzi, kuhamisha ujuzi na uelewa, na kujenga uwezo kwa taasisi za elimu nchini Ethiopia.