Zambia imeishukuru China kwa kuwa moja ya wenzi wa maendeleo waliotoa msaada wa haraka wakati nchi hiyo ilipokumbwa na mlipuko wa kipindupindu kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana mpaka katika robo ya kwanza ya mwaka huu.
Katibu wa kudumu anayeshughulikia huduma za kiufundi katika Wizara ya Afya ya Zambia, Kennedy Lishimpi amesema, mwitikio wa China uliiwezesha serikali ya Zambia kuboresha haraka upatikanaji wa maji katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo kupitia uungaji mkono katika maeneo kadhaa ikiwemo kutoa matanki ya maji.
Lishimpi pia amesema, serikali ya Zambia imetoa wito kwa kampuni za China kusaidia kuzalisha chanjo za matone za kipindupindu kama maandalizi ya msimu ujao wa mvua ambapo nchi hiyo inakuwa katika hatari zaidi ya kukumbwa na milipuko ya ugonjwa wa kipindipindu.