Burundi na China zatia saini makubaliano ya ujenzi wa jengo la wizara ya mambo ya nje
2024-09-20 08:50:42| CRI

Serikali ya Burundi na Ubalozi wa China nchini Burundi wametia saini makubaliano kwa ajili ya mchango wa ujenzi wa jengo la ghorofa 11 la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Maendeleo ya Burundi.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Maendeleo wa Burundi Albert Shingiro na Balozi wa China nchini Burundi Zhao Jiangping.

Jengo hilo litajengwa huko Gitega, mji wa kisiasa wa Burundi, na China imekubali kuliwekea jengo hilo vifaa vyote muhimu. Shingiro amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2028, na jengo hilo jipya litaunganisha idara mbalimbali za wizara katika eneo moja, likiondoa utaratibu uliopo sasa wa idara zinazotawanyika maeneo mbalimbali.