Tanzania imezindua Mpango wa Kuongeza kasi ya mauzo ya mazao nje ya nchi (HEAP) kwa lengo kuongeza mauzo ya mboga hadi kufikia dola bilioni 2 ifikapo mwaka 2030.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonyesha kuwa mauzo ya mazao ya bustani yameongezeka kwa karibu mara mbili kutoka dola za kimarekani milioni 296.5 za mwezi Julai, hadi dola za Kimarekani 437 za sasa, hasa kutokana na ongezeko kubwa la usafirishaji wa mbogamboga.
Mpango huo wenye jina la "mbio za kuelekea dola bilioni 2" ulizinduliwa wiki iliyopita mjini Arusha, na unatarajiwa kuyawezesha makampuni ya ndani kuwa shindani na kutumia kikamilifu mikataba ya biashara huria.
Mpango huo pia unalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo cha bustani kupitia kujenga uwezo, miunganisho ya kibiashara, na kufuata kwa makini viwango vya ubora wa kimataifa.