Kampuni ya China kujenga barabara ya Iringa na Hifadhi ya Ruaha nchini Tanzania
2024-09-23 11:09:57| cri

WAZIRI wa Ujenzi wa Tanzania Bw. Innocent Bashungwa, ameongoza hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 104 inayounganisha mji wa Iringa Mjini na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha nchini Tanzania.

Mradi huu ambao umekuwa ndoto ya wananchi kwa zaidi ya miaka 60, utaanza kutekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 142.56 na kampuni ya China Henan International Company Limited (CHICO) na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Waziri Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa fedha za mradi huu zitatolewa bila kukwama, na kuwa atasimamia kithabiti wa ujenzi wa mradi huo.