Zaidi ya watu 342,000 wakimbia makazi yao nchini Somalia ndani ya miezi 8
2024-09-23 08:37:05| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, mapigano, ukosefu wa usalama na mabadiliko ya tabianchi yamewafanya watu zaidi ya 342,000 kuwa wakimbizi wa ndani nchini Somalia.

Mtandao wa Ulinzi na Usimamizi ulio chini ya Shirika hilo umesema, watu 23,000 wamekosa makazi mwezi Agosti pekee, huku asilimia 43 ya watu hao ikitokana na mapigano, ukosefu wa usalama, mafuriko ama ukame.

Katika ripoti yake ya kazi iliyotolewa mjini Mogadishu, UNHCR imesema, mahitaji ya dharura kwa watu hao ni chakula, makazi, maji na huduma za afya, na kutaja mikoa ya Bari, Juba ya Kati, Gedo na Lower Juba kuwa mikoa iliyopokea wakimbizi wengi wa ndani.

Kwa mujibu wa UNHCR, wanawake na watoto ambao ni kundi lililo hatarini zaidi, wanachukua asilimia 80 ya idadi ya jumla ya wakimbizi hao wa ndani.