Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi juu ya hali ya Lebanon na Israel
2024-09-23 15:12:00| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres tarehe 22 alieleza wasiwasi juu ya hali ya mpaka wa muda kati ya Lebanon na Israel, na kuonya kuwa huenda Lebanon itakuwa “Gaza nyingine” kutokana na mapambano makali kati ya Israel na kundi la Hezbollah la Lebanon.

Wakati huohuo, mratibu maalamu anayeshughulikia masuala ya Lebanon Jeanine Hennis-Plasschaert amesema hali ya Mashariki ya Kati inakaribia kuwa  “janga” kutokana na hali ya wasiwasi kati ya kundi la Hezbollah la Lebanon na Israel, akisisitiza kuwa njia ya kijeshi haiwezi kuufanya upande wowote uwe salama zaidi.

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za diplomasia na usalama Bw. Josep Borrell Fontelles, tarehe 22 alitoa taarifa akisema Umoja wa Ulaya unafuatilia kupamba moto kwa mapambano kati ya Israel na kundi la Hezbollah, na unatoa wito kwa pande zote mbili kusimamisha vita mara moja.