Mgogoro kwenye mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan wasababisha vifo vya watu 11
2024-09-23 08:36:21| cri


Shirikisho la Madaktari nchini Sudan hivi karibuni limesema, mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) yaliyotokea jumamosi iliyopita katika mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, Al-Fashir, yamesababisha vifo vya watu 11, wakiwemo watoto watatu, na wengine 17 kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imeitaka jumuiya ya kimataifa iongeze juhudi ili hali isiwe mbaya zaidi, na kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa mapigano hayo.