Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito wa juhudi za pamoja katika bara hilo ili kukabiliana na ongezeko la tishio la amani na usalama katika bara hilo ambazo zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na matukio ya kigaidi na mapigano ya kutumia silaha.
Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa jumamosi na Kamishna wa AU anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama, Bankoye Adeoye, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, ambayo huadhimishwa kila Septemba 21.
Kamishna huyo amesema, katika baadhi ya matukio ya changamoto za amani na usalama, dhana ya ulinzi wa raia inashindwa kutekelezwa, na mauaji ya kimbari aidha yanatokea ama yanakuwa hatarini kutokea, kutokana na ukosefu wa haki, kukosa uvumilivu, kutengwa, umasikini, ukosefu wa usawa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.