Meli ya matibabu ya Jeshi la Majini la China "Peace Ark" imekamilisha kwa mafanikio ziara nyingine nchini Jamhuri ya Kongo na kuondoka kwenye Bandari ya Pointe-Noire nchini humo kuelekea Gabon, ambacho ni kituo cha nane cha jukumu hilo.
Katika ziara hiyo ya siku saba, meli hiyo ilitibu jumla ya watu 4,450, kufanya uchunguzi kwa ziada zaidi ya watu 2,300, na kufanikiwa kufanya upasuaji kwa watu 127.
Aidha, meli hiyo pia ilituma timu za wataalam kwa hospitali za mitaa kufanya matibabu ya pamoja ili kuimarisha mabadilishano ya pande zote na kuongeza uaminifu kati ya pande hizo mbili.