Shirika la Ndege la Kenya limesema limezindua kampeni ya kuvutia watalii zaidi kutoka China kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini humo.
Ofisa mwandamizi wa biashara na wateja katika Shirika hilo, Julius Thairu, amesema kampeni hiyo iliyozinduliwa jana jumatatu inajumuisha kuongeza uelewa wa Wachina kuhusu vivutio vua utalii nchini Kenya, kama vile hifadhi za wanyamapori.
Ameongeza kuwa, kwa sasa, Shirika la Ndege la Kenya linafanya safari tano kwa wiki kati ya Nairobi na Guangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Guangdong nchini China.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Bodi ya Utalii ya Kenya, watalii karibu 52,000 wa China wametembelea Kenya kwa mwaka 2023.