Xi atoa wito wa kuharakisha maendeleo katika juhudi za anga za juu za China
2024-09-24 09:20:27| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa wafanyakazi wa sekta ya anga ya juu ya China kuendelea kufanya juhudi na kuharakisha maendeleo ya sekta hiyo.

Rais Xi amesema hayo mjini Beijing akikutana na wajumbe wa wanasayansi na wahandisi wa anga ya juu walioshiriki kwenye utafiti na maendeleo ya mradi wa Mwezi wa Chang’e-6.

Rais Xi amesisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika mradi wa uchunguzi wa Mwezi yamejumuishwa busara na juhudi za vizazi vya wafanyakazi wa anga ya juu wa China, yakionesha maendeleo makubwa yaliyopatikana na nchi hiyo kwa kujitegemea kisayansi na kiteknolojia kwenye miaka ya karibuni.

Rais ametaka juhudi za kuhimiza moyo wa uchunguzi wa Mwezi unaojulikana “kufuata ndoto, kuthubutu kuchunguza, kushirikiana kushinda changamoto, na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana”, ili kuimarisha imani ya taifa na fahari ya watu wote wa China, na kujenga nguvu kubwa ya kukuza kikamilifu ujenzi wa nchi imara na kutimiza ustawi mpya wa taifa kupitia usasa wa mtindo wa kichina.