Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutuliza hali kati ya Lebanon na Israel Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutuliza hali kati ya Lebanon na Israel
2024-09-24 14:28:11| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake akisema ameshangazwa na kuongezeka kwa mvutano karibu na mstari wa utenganishaji kwenye mpaka kati ya Israel na Lebanon, na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi. Ametoa wito wa kutuliza hali mara moja na kufanya kila juhudi kutafuta suluhu ya kidiplomasia, na pande husika kulinda raia na miundombinu ya kiraia.

Pia amezikumbusha pande husika wajibu wao wa kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na mali za Umoja wa Mataifa, na kuzitaka pande zote kujitolea tena kutekeleza kikamilifu Azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama na kusitisha mara moja uhasama ili kurejesha utulivu.