Mamlaka ya kuhimiza Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA) imesajili miradi mipya 353 ya uwekezaji yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 5.5 bilioni, iliyosajiliwa katika kipindi cha miaka mitatu, ma inakadiriwa kuleta nafasi 20,000 za ajira hasa katika sekta ya utalii.
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi amesema kuanzishwa kwa miradi mikubwa kisiwani humo kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya amani na usalama inayoendelea, sambamba na sera nzuri.
Amesema uwepo wa amani na usalama kumewatia moyo wawekezaji wengi kutoka nje ya nchi kuona Zanzibar ni sehemu sahihi ya kuwekeza mitaji yao. Dk. Mwinyi pia amewataka wananchi kudumisha amani na kuendelea kuiunga mkono serikali ili uwekezaji unaoendelea katika miradi mbalimbali ya maendeleo uweze kuhimiza uchumi.