Watu 15 wauawa katika shambulizi la makombora katikati mwa Sudan
2024-09-24 08:46:32| cri

Wizara ya Afya nchini Sudan imesema, watu 15 wameuawa na wengine 61 kujeruhiwa baada ya mji wa kati wa Omdurman nchini humo kushambuliwa jana kwa makombora na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF). Wizara hiyo imesema huenda idadi ya vifo ikaongezeka zaidi.

Habari zinasema, mpaka sasa, kikosi cha RSF hakijatoa kauli yoyote kuhusu tukio hilo.