Mauzo ya nje ya kahawa kutoka Uganda nchini China yaongezeka
2024-09-24 08:39:56| CRI

Ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Kahawa ya nchini Uganda (UCDA) imesema, mauzo ya nje ya kahawa ya nchi hiyo nchini China yameongezeka mara tano kwa mwezi Agosti ikilinganishwa na mwezi Julai.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana, imeonyesha kuwa mauzo ya nje ya kahawa ya Uganda nchini China yameongezeka kutoka mabegi 2,100 mwezi Julai hadi mabegi 11,580 kwa mwezi Agosti.

Balozi mdogo wa Uganda mjini Guangzhou, China, Judyth Nsababera ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua, kuwa, ongezeko hilo ni matokeo ya uhusiano imara wa pande mbili, mkakati bora wa soko, na kuongezeka kwa ubora wa mbegu za kahawa kutoka Uganda.

Ripoti ya UCDA pia imeonyesha kuwa, China kwa sasa ni miongoni mwa vituo vya juu 20 vya kahawa ya Uganda, na kwamba, kwa ujumla, mauzo ya nje ya kahawa yamefikia dola za kimarekani bilioni 1.35 kati ya mwezi Septemba mwaka jana na mwezi Agosti mwaka huu.