WHO yatoa msaada wa vifaa 5,000 vya upimaji wa Mpox kwa Uganda
2024-09-25 08:38:08| cri

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa msaada wa vifaa 5,000 vya upimaji wa Mpox kwa Uganda ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Katika taarifa iliyotolewa jana, WHO imesema vifaa hivyo vitasaidia Wizara ya Afya ya Uganda katika upimaji sahihi na wa wakati unaofaa, ambao ni muhimu katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo unaoambukiza kwa kasi kubwa.

Baada ya kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Agosti, Uganda imesajili kesi 24 za mpox katika wilaya 10, na kati ya hizo, wagonjwa 13 wamepona huku 11 bado wamelazwa hospitalini.