Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat tarehe 24 Septemba alitoa taarifa akieleza wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya sehemu nyingi za Sudan hususan mji wa Al-Fashir, Darfur Kaskazini, pia alitoa wito kwa Jeshi la Sudan, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wafuasi wa pande mbili wasitishe vita mara moja bila ya masharti.
Taarifa imesema mgogoro wa Sudan hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kijeshi, na vita itaongeza tu mateso kwa watu wa Sudan. Moussa Faki amezihimiza pande zote zisimamishe vita mara moja, kutandika njia kwa ajili ya mazungumzo ya kisiasa ya pande zote, kuondoa mzizi wa mapambano, na kurejesha amani na utulivu nchini Sudan. Pia amesisitiza kuwa Umoja wa Afrika utaihimiza Sudan kusitisha vita na kurejesha amani kupitia mfumo wa kamati ya ngazi ya juu ya masuala ya Sudan.