China yapinga vitendo vyovyote vya kudhuru raia
2024-09-25 09:20:05| cri



Wizara ya Afya nchini Lebanon juzi ilisema, mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa siku hiyo na Israel dhidi ya Lebanon yamesababisha vifo vya watu 492 na wengine 1,645 kujeruhiwa. 

Akizungumzia shambulio hilo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian jana alipokutana na wanahabari amesema, China inapinga vitendo vya kukiuka mamlaka ya kitaifa na usalama wa Lebanon, na kulaani vitendo vyovyote vinavyodhuru raia.

Bw. Lin amesema China inazitaka pande husika zichukue hatua na kupunguza mvutano, kuzuia hali ya wasiwasi ya kanda hiyo iwe mbaya zaidi, na kulinda utulivu wa kikanda na usalama wa maisha ya watu.