Ofisi ya Habari na Uhusiano na Umma ya Jeshi la Senegali jana imesema, Jeshi la Majini la nchi hiyo limepata miili 30 kwenye boti ya wahamiaji katika bahari karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar jumapili jioni.
Taarifa hiyo imesema kwa kuwa miili hiyo imeharibika, ni vigumu kuitoa, kuitambua na kuihamisha.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, boti hiyo iliondoka katika mji wa Mbour, magharibi mwa Senegal, katikati ya mwezi Agosti na ilikuwa ikielekea Hispania, na ilipoteza mawasiliano baada ya kuondoka.
Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.