Viongozi wa Afrika watoa wito wa pamoja wa kuwa na nafasi zaidi ya maendeleo
2024-09-26 08:49:48| CRI

Viongozi wa nchi na serikali za Afrika wameshiriki katika mjadala wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakieleza haja ya pamoja kuwa nchi zao zitaendelea kwa kasi na kwa usalama katika njia za maendeleo halisi huku zikitarajia Umoja huo utajitahidi kadiri uwezavyo kuzisaidia kukabiliana na vikwazo vilivyopo sasa na kujiandaa kwa siku za baadaye.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Ado anayehudhuria Mkutano huo amesema, kuna fursa nyingi barani Afrika, na kwamba bara hilo linatakiwa kutafuta njia mpya za maendeleo. Ameongeza kuwa, si rahisi kuzungumzia changamoto za sasa za bara hilo bila kujadili mkanganyiko ulioko ndani ya taasisi hiyo ya kimataifa.

Rais wa Mkutano wa 79 wa Baraza la Umoja wa Mataifa Philemon Yang amesema katika hotuba yake ya ufunguzi wa mjadala huo, kwamba utakuwa ni kipaumbele chake kwa muda wa urais wake, na kuongeza kuwa, Afrika ni moja ya vipaumbele vya Umoja wa Mataifa, ambao unapaswa kuiunga mkono Afrika.