Kenya yalitaka bara la Afrika kuungana ili kufungua fursa za uchumi wa kidijitali
2024-09-26 08:51:13| CRI

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesisitiza haja ya dharura ya kufungua fursa nyingi zinazotolewa na uchumi wa kidijitali kwa nchi za Afrika, akisisitiza uwezekano wa kutoa fursa za ajira na kuboresha sekta ya huduma.

Akizungumza katika Mkutano wa Shirikisho la Kimataifa la Bustani za Sayansi na Maeneo ya Uvumbuzi (IASP) uliofanyika mjini Nairobi, Gachagua amesema bara hilo lina fursa ya kuwa nguvu kubwa ya teknolojia duniani kwa kutumia uvumbuzi na moyo wa ujasiriamali wa vijana.

Amesema kwa kuendeleza vituo vya sayansi, teknolojia na uvumbuzi, anaamini kuwa Afrika itakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kukabiliana na masuala muhimu kama umasikini, njaa, ukosefu wa ajira kwa vijana, magonjwa na mgogoro wa kimazingira.