Zimbabwe kuimarisha ushirikiano wa FOCAC kwa ajili ya mambo ya kisasa
2024-09-26 08:49:04| CRI

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa nchi hiyo itaimarisha ushirikiano ulioanzishwa chini ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ili kuharakisha mchakato wa mambo ya kisasa, mapinduzi ya viwanda na kutekeleza mageuzi ya kiuchumi yanayozingatia watu.

Akizungumza katika Mkutano wa 378 wa Chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF mjini Harare kuwa, Rais Mnangagwa amesema ziara yake ya kiserikali nchini China na kushiriki katika mkutano wa FOCAC imetoa fursa ya kuimarisha uhusiano kati yake na China katika nyanja mbalimbali.

Rais Mnangagwa pia amesema licha ya kuangazia uchumi na biashara, ni muhimu kutafuta ushirikiano na China katika sekta nyingine zikiwemo michezo, utamaduni, utalii na vyombo vya habari.