Wizara ya Biashara ya China imesema kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa huduma ya China imefikia yuan trilioni 4.23 (sawa na dola milioni 601.8 za kimarekani), ambayo imeongezeka kwa asilimia 14.7 ikilinganishwa na mwaka jana, na thamani ya uagizaji na uuzaji wa huduma ya ujuzi imechukua takriban asilimia 40.
Kuanzia mwaka huu, China imejenga vituo vipya 12 vya biashara ya kiutamaduni kwa nje, hatua ambayo imetoa uhakikisho wa huduma kwa makampuni ya utamaduni na utalii ya China yanayopanua masoko ya nje na kwa makampuni ya nje yanayowekeza nchini China.