Rais wa Guinea-Bissau asifu mapambano ya Afrika dhidi ya malaria
2024-09-26 08:47:28| cri



Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló jana kwenye Baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema, Muungano wa Viongozi wa Afrika wa Kupambana na Malaria (ALMA) umepata maendeleo makubwa katika mazingira magumu sana ya dunia, na kujitahidi kupata uungwaji mkono wa Mfuko wa Kimataifa. 

Rais Embalo amesema, Muungano huo umefanya kazi na sekta binafsi ili kukuza uzalishaji wa dawa na vyandarua ili kukabiliana na malaria, pia ulihimiza uhamishaji wa teknolojia kwa makampuni ya Afrika. Vilevile ulizindua bodi na mifuko ya kukomesha malaria na kuwaunga mkono vijana kupambana na malaria.