Hivi karibuni, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito katika mkutano wa kilele wa siku za baadaye wa Umoja wa Mataifa kwamba watu wa sehemu mbalimbali duniani wanataka siku za baadaye zenye amani, heshima na ustawi, wanahimiza kuchukua hatua za dunia nzima kutatua masuala ya msukosuko wa tabianchi, hali isiyo usawa na kukabiliana na hatari mpya zinazokabili kila mmoja. Bw. Guterres amezitaka nchi mbalimbali kuimarisha umoja na kukabiliana kwa pamoja na changamoto na migogoro.
Mkutano huo wa kilele ni moja kati ya mikutano muhimu ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa. Kwa nini “Zama Zijazo” imekuwa mada kuu ya mkutano huo? Chanzo cha moja kwa moja ni kuwa msukosuko wa dunia unaendelea kuzidi, hatari zinazokabili binadamu ni kubwa zaidi katika historia ikiwemo vita kati ya Russia na Ukraine, Palestina na Israel, na mikwaruzano kati ya Lebanon na Israel. Wakati huohuo, changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, mgogoro wa wakimbizi na matumizi ya teknolojia mpya. Binadamu wanahitaji siku za baadaye za namna gani? Na siku nzuri zaidi za baadaye zitajengwaje?
Katika mustakabali huo, viongozi na wakuu 130 wa serikali na nchi wamejumuika jijini New York kujadili mwelekeo wa kusonga mbele katika siku za badaaye. Katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa kilele, pande mbalimbali zimepitisha “Mkataba wa Zama Zijazo” na viambatisho vyake “Mkataba wa Kimataifa Kuhusu Dijitali” na “Azimio la Vizazi Vijavyo”. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mijadala ya miaka miwili, yakionesha nia ya pande mbalimbali kufanya mageuzi ya usimamizi wa kimataifa, kustawisha mfumo wa pande nyingi, kukabiliana na changamoto. Kwa mujibu wa maudhui yake, makubaliano hayo yanalenga ajenda tano ikiwemo maendeleo endelevu, amani na usalama, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, vijana na vizazi vya siku za baadaye, usimamizi wa dunia na kutoa mipango ya hatua 56, huku yakifungua zama mpya ya pande zote na kuchukuliwa kama waraka muhimu unaochora ramani ya maendeleo ya ya dunia katika siku za baadaye.