Meli ya hospitali ya “Peace Ark” ya Jeshi la Majini la China yawasili Gabon
2024-09-27 10:12:07| cri

Meli ya hospitali ya “Peace Ark” ya Jeshi la Majini la China Septemba 26 ilitia nanga katika bandari ya Owendo mjini Libreville na kuanza ziara ya siku saba nchini Gabon, ikiwa ni ziara yake nyingine nchini humo baada ya miaka saba.

Katika ziara hiyo, Meli ya hospitali ya “Peace Ark” itatoa upimaji na matibabu kwa wagonjwa, na pia itatuma kikundi cha wataalamu kwenda kwenye hospitali za huko kushiriki katika huduma za matibabu. Aidha, wanajeshi wa meli hiyo wanatarajiwa kutoa huduma za afya katika shule, na kushiriki kwenye mechi ya kirafiki na wanajeshi wa Gabon.