Mapigano makali yametokea kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) katika maeneo mengi yanayodhibitiwa na kikosi hicho katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Chanzo cha kijeshi cha Sudan kimeliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwamba, jeshi hilo lilifanya mashambulizi kwenye maeneo mengi ya kimkakati katikati ya Khartoum jana, kwa lengo la kuwafukuza wapiganaji wa kundi la RSF kutoka katika maeneo hayo.
Pia chanzo hicho kimesema operesheni hiyo ni kubwa zaidi ya mashambulizi iliyoanzishwa na jeshi la Sudan mjini Khartoum.
Hakuna upande wowote uliotoa taarifa kuhusu vifo ama majeruhi kutokana na mapigano hayo.