Rais wa Kenya alaani msimamo wa upande mmoja na utandawazi wa kijeshi
2024-09-27 08:43:37| cri



Rais William Ruto wa Kenya jana kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amezilaumu nchi nyingi zaidi kwa kuchagua msimamo wa upande mmoja na utandawazi wa kijeshi, badala mazungumzo na diplomasia, hatua ambayo imezidisha hali ya wasiwasi, na kuharibu uaminifu kuhusu mfumo wa pande nyingi duniani.

Rais Ruto amesema changamoto hizo ni ngumu, zinahusiana na zinaongezeka kwa kasi, na kuongeza kuwa, mabadiliko ya tabianchi yanaochochea zaidi ukosefu wa usalama na mapigano duniani.