Maofisa wa serikali na taasisi za kimataifa watoa wito wa kuimarisha usimamizi wa data barani Afrika
2024-09-27 10:14:41| cri

Maofisa kutoka serikalini na taasisi za kimataifa wametoa wito wa kuongezeka kwa matumizi ya data katika utungaji sera, wakisisitiza umuhimu wa kutumia maarifa yanayotokana na data ili kuhimiza ufanyaji maamuzi bora katika sekta mbalimbali. Wito huo umetolewa kwenye ufunguzi wa Kongamano la pili la Innovate Africa lililofanyika mjini Kigali.

Mkurugenzi wa Takwimu katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Samson Babatunde Omotosho amesema bila ya usimamizi mzuri wa data, kutakuwa na upungufu mwingi unaoweza kufanya utungaji sera kuwa mgumu na kudhoofisha imani katika mifumo ya serikali.

Bw. Omotosho amesisitiza kuwa umuhimu kukuza ushirikiano thabiti kati ya watayarishaji wa data na watumiaji, na kusema uwekezaji mkubwa katika ukusanyaji na uchanganuzi wa takwimu hakutakuwa na maana, kama hautachangia kwenye utungaji wa sera, kwani hautaleta athari zinazoonekana kwa maisha ya watu.