Tanzania yawahakikishia wazalishaji umeme wa uhakika
2024-09-27 10:15:16| cri

Serikali ya Tanzania imewahakikishia wazalishaji kuwa kutakuwa na umeme wa kutegemewa kusaidia uzalishaji wa ndani wa viwanda.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw. Doto Biteko amesema Tanzania sasa ina umeme wa kutosha baada ya hivi karibuni kuongezwa umeme kutoka kwa Mradi wa Umeme wa Maji Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Bw. Biteko ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya pili ya Maonesho ya Kimataifa ya Wazalishaji Tanzania (TIMEXPO) 2024, kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Amesema licha ya masuala madogo madogo yaliyojitokeza katika miezi ya hivi karibuni, ambayo yalisababisha kukatika kwa umeme, uzalishaji wa umeme unaotokana na maji kwa sasa umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na hivyo kupunguza utegemezi wa gesi katika uzalishaji wa umeme.