Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema thamani ya miradi ya uwekezaji imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 hadi kufikia dola bilioni 1.61 katika robo iliyoishia Juni 2024.
Kwenye ripoti iliyotolewa hivi karibuni, TIC imesema ongezeko la mtaji linaonyesha nia inayoongezeka ya kuwekeza nchini Tanzania, kutokana na miradi 198 iliyoandikishwa katika kipindi hicho, tofauti na miradi 129 yenye thamani ya dola bilioni 1, ya robo iliyopita.
Mkurugenzi mtendaji wa TIC Bw Gilead Teri amesema uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) umechangia sehemu kubwa ukiwa na ongezeko la asilimia 136.35 au dola za kimarekani milioni 938.32, ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 681.48 milioni katika robo kama hiyo kwa mwaka jana.