Kiongozi wa RSF asema RSF wako tayari kusitisha mapambano
2024-09-27 22:12:27| cri

Kiongozi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) cha Sudan Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo jana Alhamisi alisema, kikosi chake kiko tayari kusitisha mapambano katika nchi nzima, na kinapenda kushiriki kwenye mazungumzo shirikishi yanayohusisha pande zote za Sudan, ili kutatua msukosuko uliopo kwa njia ya kisiasa.

Jenerali Dagalo amesema, kikosi cha RSF kimeahidi kufanya operesheni za kijeshi kwa mujibu wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa, kulinda usalama wa raia na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia watu wenye mahitaji kote nchini. Jenerali Dagalo pia amepinga mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan kuiwakilisha Sudan kwenye Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.