Xi asisitiza kuimarisha umoja wa taifa la China
2024-09-27 15:50:34| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuimarisha na kuendeleza umoja wa taifa la China.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, ametoa wito huo kwenye mkutano wa kitaifa uliofanyika leo Ijumaa jijini Beijing kwa ajili ya kuwapongeza watu waliotoa mifano ya kuigwa katika kuendeleza umoja wa watu kutoka makabila mbalimbali nchini.

Rais Xi pia amehimiza juhudi za kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya taifa la China yenye mustakabali wa pamoja.