Timu ya madaktari wa China yafanya upasuaji bure nchini Ghana
2024-09-27 08:35:23| CRI

Mradi wa hisani wa kufanya tiba ya upasuaji wa bure nchini Ghana umezinduliwa tena jumatano wiki hii na timu ya madaktari wa China kwa kuungwa mkono na kampuni za China na mashirika ya hisani.

Chini ya mradi huo unaoitwa “Upasuaji Mdogo nchini Ghana na Kuona Dunia Nzuri,” timu ya 13 ya madaktari wa China wataendelea kutoa tiba ya bure ya upasuaji kwa wagonjwa wa mtoto wa jicho, na pia upasuaji wa bure wa laparoscopic katika Hospitali ya Urafiki wa China na Ghana iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.

Mkurugenzi wa ushirikiano wa afya katika Idara ya Uratibu wa Kiufundi iliyo chini ya Wizara ya Afya ya Ghana, Hafiz Adam Taher amewashukuru madaktari wa China kwa kuleta matumaini kwa Waghana kupitia huduma zao.

Naye Balozi wa China nchini Ghana Tong Defa aesema, tiba na afya ni mambo mawili makubwa ya ushirikiano kati ya China na Ghana, na kwa sababu hiyo, China imekuwa ikiunga mkono kidhahiri maendeleo ya mfumo wa afya wa Ghana kwa miaka mingi.