Ripoti ya “Viashiria vya kiwango cha uvumbuzi (GII) duniani kwa mwaka 2024” iliyotolewa jana na Shirika la Haki Miliki Duniani imesema, kiwango cha uvumbuzi cha China kilipanda kwa nafasi moja kuliko mwaka jana na kufikia nafasi ya 11 duniani, na kuwa moja ya makundi ya kiuchumi ambayo kiwango cha uvumbuzi kiliongezeka kwa kasi zaidi katika muongo uliopita.
Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, China ni kundi pekee la kiuchumi lenye mapato ya kati miongoni mwa makundi 30 ya kiuchumi yanayoshika nafasi 30 za mwanzo kwa kiwango cha uvumbuzi duniani.
China inashika nafasi ya kwanza katika viashiria nane kati ya 78 vya uvumbuzi.