Leo jumapili ya Septemba 29, China inafanya sherehe kutoa heshima za hadhi ya juu zaidi za serikali kabla ya maadhimisho ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Wakisindikizwa na msafara wa magari, watunukiwa nishani za taifa na vyeo vya heshima vya kitaifa wamekwenda kwenye Jumba la Mikutano ya Umma wa Beijing. Msafara wa magari uliobeba wapokeaji wa nishani za taifa na vyeo vya heshima vya kitaifa, umeambatana na wasindikizaji wa pikipiki kuelekea kwenye Jumba la mikutano ya umma ambako sherehe imefanyika asubuhi.